Aliyekuwa mchezaji wa Arsenali, Emmanuel Ebue aelezea jinsi mkewe alimfanya kuwa maskini

September 2024 · 2 minute read

- Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Arsenali, Emmanuel Eboue amezungumzia matukio yaliyomfilisisha kabisa licha ya kuwa mchezaji maarufu

- Eboue ambaye ni raia wa Ivory Coast alizungumza jinsi mkewe alichangia kufilisika kwake katika mahojiano na French TV

Aliyekuwa mchezaji wa klabu cha soka cha Arsenali, Emmanuel Eboue amefunguka kuhusu yale yaliyomfanya kuwa fukara licha ya kuwa mchezaji wa kulipwa katika ligi kuu ya Uingereza.

Mchezaji huyo wa miaka 34 alisema kuwa licha ya kung'ang'ana sana kuona nyota yake inang'aa, alipitia mengi yaliyomwacha hoi.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Mpango wa kando wake Diamond kutoka Rwanda aonekana akiwa na viatu vya bei ghali

Eboue alisema kuwa alipoteza katika kesi yake na mkewe, Aurelie ya kutalakiana na hivyo kupoteza mali yake yote. Aliongeza kusema kuwa hajakuwa akiwaona wanawe watatu.

Akiongea katika mahojiano hayo, Eboue alifichua kuwa talaka hiyo ilimfanya kusalia mpweke. Alielezea kuwa yeye yu tayari kuchezea popote soka, la maana kwake likiwa ni kujiona amerejea uwanjani.

Habari Nyingine: Tunataka Jubilee kukubali kuwa haikushinda uchaguzi-Raila Odinga

"Huwa sitazami TV wakati ninapokuwa nyumbani, kama nikiona marafiki zangu wanacheza mpira wa miguu ninawafurahia- lakini ndani kabisa ndani yangu nalia machozi. Nilipopata talaka niligundua kuwa hakuna kitu kilichosalia katika akaunti yangu ya benki. Sijawahi kufikiri kwamba mtu aliyekuwa na mimi, na kuwa na watoto pamoja nami, anaweza kufanya hivyo. Unaona mambo kama hayo yanayotokea katika filamu, lakini sijafikiri kwamba inaweza kutokea kwangu," Asema Eboue.

Eboue alitumia miaka saba katika Ligi Kuu na akapata mamilioni ya pesa wakati huo akichezea.

"Nilipata euro milioni nane. Nilituma nyumbani milioni saba. Chochote ambacho ananiambia nisaini, nasaini. Fedha nilizopata, nilipeleka kwa mke wangu kwa ajili ya watoto wetu." Alisema Eboue

Read ENGISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4J0hJRmmKWhqZq4tsPAZqScoJWvrqu1jLCYZpmiqLKvrcuiZJ6lnZa7trHLZpybrZVirqa4xLOcmmWanru0tYymop6vlWKurbXMn5insZFiuLbDwGakmqubnruqesetpKU%3D